Mtalaamu wa kukarabati nakala za vitabu vya kale katika Msikiti wa Al-Aqsa, Yusuf Al-Uzbeki, anaamini kuwa mwandishi wa nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu ni Muhammad bin Al-Hasan bin Al-Hussein bin Zainul Abidin Ali bin Al-Hussein bin Ali bin Abi Talib (as).
Mwanaakiolojia wa Msikiti wa Al-Aqsa, Ismail Sharawneh ameiambiai Al Jazeera Net kuwa nakala hiyo iliandikwa kwa hati za Kikufi kwenye ngozi ya swala (mnyama) kwa kutumia wino mweusi. Herufi zake zilitengenezwa na kuwekwa alama kwa mtindo wa Abul-Aswad al-Du'ali.
Ameongeza kuwa nakala hii ni ya kipekee miongoni mwa nakala nyinginezo za Qur'ani katika Makumbusho ya Kiislamu kwa kuwa inatumia herufi za abjadi kama namba, kwani Aya za Qur'ani hazikuwekwa nambari kwa kutumia tarakimu, bali zilihesabiwa kwa kutumia herufi za Kiarabu.
Kwa sasa Msikiti wa al Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, na mji mtakatifu wa Quds kwa ujumla unakaliwa kwa mabavu na utawala katili na dhalimu wa Israel.
342/
Your Comment